Kinana kuendelea nafasi ya ukatibu mkuu wa CCM

0
133

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Abdurahman Kinana ataendelea kuwa katibu mkuu wa chama hicho.

Taarifa kwamba ataendelea kuhudumu zimepokelewa kwa shangwe na vigelegele na wajumbe wanaohudhuria mkutano mkuu wa tisa wa chama hicho mjini Dodoma.

Rais Magufuli ambae ndiye mwenyekiti wa sasa, alitangaza uamuzi huo wa Bw Kinana kwa wajumbe hao takriban 1,900.

Katika hotuba yake ya ufunguzi, Rais Magufuli alimshukuru katiba mkuu wake na kusema ana imani naye katika utendaji wake wa kazi.

Kinana ambaye amekuwa akishikilia wadhifa huko tangu serikali ya awamu ya nne, na wachambuzi wamekuwa wakimuona kama kiungo muhimu sana katika kuleta mabadiliko ndani ya Chama.

Awali kulikuwa na tetesi kwamba Kinana angeachia nafasi hiyo kwa lengo la kutaka kustaafu.

Kinana, mbali ya kuwa mwanajeshi mstaafu, ana uzoefu mkubwa katika masuala ya utawala na siasa.

 

LEAVE A REPLY