Kinachondelea msiba wa Mama wa P. Funk

0
17

Mtayarishaji wa muziki nchini, Paul Matthysse maarufu kama P Funk Majani amefiwa na mama yake mzazi aitwae Aunt Sheilah ambaye amefariki nchini Uholanzi.

Kaka wa marehemu Fadhili Kiholi amesema mipango ya mazishi inaendelea kufanywa, na kwa sasa msiba upo Kilosa mkoani Morogoro na ndipo atazikiwa baada ya kuurudisha mwili wa marehemu.

Amesema kuwa Mpaka sasa hivi mwili bado upo Uholanzi, tunafanya michakato ya mwili kurejea hapa nchini. Tutaondoka leo jioni na taratibu zote tunatarajia kuzifanya wiki ijayo.

“Marehemu alikuwa akiishi Tanzania na alienda Uholanzi mwezi wa tisa mwaka jana kama sehemu ya matibabu.

Huwa anaendaga mara kwa mara Uholanzi ila muda huu amekaa kidogo, pia mipango ya mazishi itafanyika Kilosa Morogoro kwenye ardhi aliyozaliwa,” amesema Kiholi.

LEAVE A REPLY