Kim Kardashian Kendall kuuza sura kwenye Ocean’s Eight

0
106

Filamu mpya ya Ocean Eight ambayo itahusisha waigizaji wa kike pekee imeongeza idadi ya mastaa watakaoshiriki movie hiyo kwa kuwaingiza ndugu wawili wa familia ya Kardashian.

Ndugu hao Kim Kardashian na mdogo wake Kendall Jenner watashiriki kwenye filamu hiyo ingawa watacheza kama waigizaji wadogo ambao hawatakuwa na athari kubwa kwenye mtiririko wa matukio.

Filamu hiyo ambayo ni mfululizo wa filamu za Oceans ndani ya kipindi cha miaka 17 ni ya nne ikitanguliwa na Ocean’s Eleven, Twelve and Thirteen.

Mastaa hao wawili, Kardashian Jenner walionekana jijini New York ambapo iliripotiwa kuwa walikuwa wakiigiza sehemu ya filamu hiyo.

Mastaa wanaotarajiwa kucheza kama waigizaji viongozi au waigizaji muhimu kwenye filamu hiyo ni pamoja na staa wa Pop, Rihanna na wengine ni pamoja na Sandra Bullock, Cate Blanchett na Anne Hathaway.

Filamu hiyo inatarajiwa kutoka mwezi Juni mwaka 2018.

LEAVE A REPLY