Killy akanusha kukata mawasiliano na Kings Music

0
45

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Killy kutoka lebo ya Konde Gang amekanusha kukata mawasiliano na wasanii wenzake aliokuwa nao lebo ya Kings Musici chini ya Alikiba.

Killy amesema kuwa hajafuta na hawezi kufuta namba za wasanii aliowaacha kwenye lebo hiyo kwani bado ni familia yake ila kilichobadilika ni kuhamia upande mwingine katika harakati za kimuziki.

Killy ameamua kusema hayo baada ya tetesi zikidai kuwa amefuta namba za wasanii wa Kings Music Records na hawana mawasiliano tena baada ya kusainiwa Konde Gang ya Harmonize.

“Hizi ni harakati na maamuzi pia ni muendelezo wa maisha ya muziki, Konde Gang wamenipokea kwa mikoni miwili, kuna upendo sana na tunaishi kifamilia kabla ya kazi, sijafuta namba ya mtu yeyote kila kitu kipo vilevile wale bado ni ndugu zangu na hatujagombana sijaongea na Alikiba ila Abdukiba nazungumza naye” amesema Killy

Killy na Cheed walitangaza kujitoa Kings Music Records ya Alikiba siku ya Aprili 14, 2020 ambapo kwa sasa wapo lebo ya Konde Gang chini ya msanii Harmonize.

LEAVE A REPLY