Kikwete asikitishwa na kifo cha Mzee Kingunge

0
192

Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa hana maneno ya kutosha kubeba uzito wa simanzi zake kwa Mwanasiasa Mkongwe Kingunge Ngombali Mwiru.

Dkt Kikwete ameeleza kuwa Mzee Kingunge ni moja ya walezi wake waliomlea kisiasa na wametoka mbali.

“Nimepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa za kifo cha Mzee Kingunge Ngombare Mwiru.Sina maneno ya kutosha kubeba uzito wa simanzi zangu.Mzee huyu ni moja ya walezi wangu kisiasa. Tumetoka nae mbali. Natoa pole zangu kwa familia na Watanzania wote. Alale kwa amani,“ ameandika Dkt. Kikwete katika ukurasa wake wa Twitter.

Kingunge Ngombale-Mwiru amefariki dunia leo katika hospitali ya taifa Muhimbili.

Taarifa hizo zimethibitishwa na Mtoto wake Kinje Ngombale kuwa Baba yake amefariki usiku wa kumakia leo.

Kingunge Ngombale Mwiru ni ni mstaafu ambaye katika maisha yake toka ujana wake amelitumikia Taifa mpaka hata ngazi za juu kabisa kama vile kuwa Mkuu wa Mkoa, Mbunge na hata Waziri.

 

LEAVE A REPLY