Kikwete afunguka changamoto anazokumbana nazo kwenye kilimo

0
161

Rais mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Mrisho Kiwete amezungumzia shughuli za kilimo anazozifanya huku akianika changamoto mbalimbali zinazomkabili kwenye kilimo baada ya kustaafu.

Akizungumza jana Ijumaa muda mfupi mara baada ya Mwenge wa Uhuru kufika kwenye shamba lake la mananasi lenye ukubwa wa eka zaidi ya 200 mkoani Pwani.

Kikwete amesema kuwa ingawa kilimo alianza tangu mwaka 1989, lakini suala la palizi na ukosefu wa maji ni moja ya changamoto anazokabiliana nazo.

Amesema kuwa ingawa mananasi yanazaa vizuri kama yatapata huduma zote kikamilifu, lakini mkulima anaweza kupambana na ukosefu wa masoko pindi unapofikia msimu wa mavuno.

Amesema kuwa mikakati aliyonayo kwa kushirikiana na taasisi na wakulima mbalimbali ni kutafuta mbegu za mananasi kutoka nje ya nchi na mkakati wa kuanzisha kilimo cha mananasi kwa njia ya umwagiliaji hali aliyosema itawainua wakulima wengi na kujikwamua katika janga la umaskini.

Kwa upande wake Mkimbiza Mwenge wa Uhuru kitaifa, Amour Hamad Amour amempongeza Kikwete kwa kuonyesha mfano bora hususan kuendeleza kilimo cha mananasi huku amiwahimiza Watanzania kuiga mfano huo.

 

 

LEAVE A REPLY