Kikwete achuguliwa kuwa mwenyekiti wa Baraza la wakimbizi

0
148

Rais mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amechaguliwa kuwa mwenyekiti mwenza wa Baraza la wakimbizi.

Rais Kikwete amechaguliwa kushika wadhifa huo wakati akiwa bado mwenyekiti wa jopo la ngazi ya juu kuhusu mwitikio wa Kimataifa wa majanga ya afya.

Mwaka juzi aliyekuwa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) Ban Ki Moon aliyemteua Kikwete kushika wadhifa huo.

Kwasasa amekuwa kiongozi tena wa ngazi ya juu wa Baraza hilo la Mataifa ambapo atakuwa na mwenyekiti wenza ambao ni Hina Jilani kutoka Pakistani na Ritha Sussmuth kutoka Germany.

Baraza hilo la limeanzishwa mwaka 1951 ili kushughulikia masuala ya wakimbizi duniani kote kutokana na tatizo la wakimbizi.

LEAVE A REPLY