Kifo? Rais Erdogan ashindwa kukanusha kuhusu adhabu ya kunyonga

0
162

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ameshindwa kukanusha iwapo atarudisha adhabu ya kunyonga nchini humo katika kipindi hiki ambapo watuhumiwa wa njama za kuipindua serikali yake wapo mahakamani kujibu mashaka ya uhaini ambayo kwenye nchi nyingi adhabu yake huwa ni kifo.

Watu 27 wengi wao wakiwa wanajeshi wa jeshi la Uturuki wamefikishwa mahakamani muda mfupi uliopita mjini Ankara wakikabiliwa na mashtaka mbalimbali huku kubwa zaidi likiwa ni kula njama za kuipindua serikali.

Miongoni mwa washtakiwa ni pamoja na jenerali Akin Ozturk aliyewahi kuwa kamanda wa kikosi cha anga cha Uturuki anayelaumiwa vikali na rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan kwa kuongoza mapinduzi yaliyoshindwa.

Rais Erdogan amejinasibu kuendelea kuwatafuta na kuwatia nguvuni watu wote waliokula njama ya kumpindua ambapo hadi sasa zaidi ya watu 6,000 wameshakamatwa ambamo miongoni mwao ni maafisa wa juu wa jeshi.

Wizara ya mambo ya ndani ya Uturuki imewafuta kazi watumishi 8,777 kati yao askari wakiwa 7,899.

Jaribio hilo la mapinduzi nchini Uturuki limesababisha vifo vya watu 290 na wengine zaidi ya 1,400 kujeruhiwa.

Waziri mkuu wa Uturuki Binali Yildirim ametangaza kuwa waanzilishi wa jaribio hilo watalipa kwa maumivu makubwa huku rais wa Uturuki akijinasibu kuondoa virusi kwenye taasisi zote za serikali.

People react as bodies draped in Turkish flags are seen on the ground during an attempted coup in Ankara

 

LEAVE A REPLY