Kiba kufunga mwaka na shoo mbili

0
101

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Alikiba amefunguka na kusema kuwa anatarajia kufanya shoo mbili za kufunga mwaka ndani ya mwezi wa Disemba.

Kupitia akaunti yake ya Instagram Kiba ameweka wazi kwa kusema kuwa mwisho wa mwaka huu atafanya shoo kwa ajili ya kufunga mwaka na mashabiki wake ambao walimsapoti kipindi cha chote cha mwaka huu.

Kiba amefunga hayo ikiwa leo ni siku yake ya kuzaliwa ambapo amemshukuru mungu kwa kufikia mwaka mwingine.

Kupitia akaunti yake ya Instagram Kiba amefunguka ameandika yafuatayo ” Ikiwa leo ni siku yangu ya kuzaliwa namshukuru Mungu kwa kuendelea kunibariki katika kila jambo na namshukuru kwa kunipa mashabiki wanaonipa support ya dhati kabisa. Shukrani zangu kwa mashabiki mwaka huu katika #FungaMwakaNaKingKiba zinakuja na show mbili kubwa ndani ya December 2018.”

LEAVE A REPLY