Kiba aitambulisha rasmi King’s Music

0
148

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Alikiba amewatambulishwa wasanii wanne ambao watakuwa chini ya lebo yake ya King’s Music itakayoanza kufanya kazi hivi karibuni.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram Alikiba ameweka picha za wasanii hao ambao watakuwa chini ya lebo yake hiyo inayoongozwa na yeye mwenyewe kwa kila kitu.

Wasanii hao ni 2ga K, Killy, Rasheed pamoja na Abdul Kiba ambaye yeye alikuwa anafanya kazi na msanii huyo toka siku za nyuma.

Baada ya utambulisho huo Mwanamuziki huyo na kundi hilo tayari wameachia wimbo wao mpya unaokwenda kwa jina la ‘Mwambie Sina’.

Baada ya kuposti picha za wasanii wake hao, baadhi ya mashabiki wake wamesema kuwa walikuwa wanasubili sana ujio wa lebo yake hiyo mpya.

LEAVE A REPLY