Khasim Mganga amwagia sifa Mbosso

0
247

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Khassim Mganga amefunguka na kusema kuwa anatamani sana kuwepo na wasani wengi kama Mbosso kwani ana uwezo mkubwa sana wa kuimba.

Msanii huyo amemwagia sifa Maromboso kutokana na uwezo wake wa kuimba toka alivyoanza kufanya muziki kama solo artist baada ya kuvunjika kwa kundi la Yamoto Band.

Khassim Mganga amesema kuwa amekuwa akimfatilia mbosso kwa muda tangu ameanza kufanya kazi na amekuwa na bidii katika kazi na anatamani kuwa wasanii wengine wazaliwe wawe kama Mboso.

Pia Khassim Mganga amesema kuwa kuwepo kwa wasanii kama Mboso hakumpi changamoto bali kuna mpa moyo kuwa muziki unazidi kusonga na yeye anatoa baraka zake.

Msanii huyo kwasasa ameahamishia makazi yake jijini Dar es Salaam akitokea mkoani Tanga pamoja na kampuni yake anayoifanyia kazi ya Manza Bay.

LEAVE A REPLY