Khadija Kopa amewata wadhamini kuwekeza kwenye muziki wa Taarab

0
507

Malkia wa muziki wa taarabu nchini, Khadija Kopa amewataka mameneja kujitokeza kuwadhamini na kuwasimamia wasanii wa taarabu ili waweze kufanikisha muziki wa tarabu kufika kimataifa.

Khadija Kopa amesema kwa sasa anahitaji kupata wadhamini ili kuweza kufanya video nzuri kwani yeye anajua kuimba lakini hajui maswala ya uongozi hivyo anatamani kupata usimamizi ili kuweza kutengeneza kazi nzuri zaidi.

 

Pia amesema  kwa sasa anajipanga ili arudi na muziki wa kisasa na kuwasihi mameneja wanaotamani kufanya kazi na yeye wajitokeze wasiogope umaarufu wake.

Mwanamuziki huyo ambaye kwasasa anatamba na kundi lake la Ogopa Kopa Modern Taarab amendelea kusema kuwa ili muziki wa taarab uendelee na kufika kimataifa lazima wadhamini wajitokeze kuusapoti muziki huo.

Mkali huyo amepata umaarufu kupitia muziki huo wa taarab kutokana na kuanza kuimba kwake miaka mingi lakini hadi sasa anaendelea kufanya vizuri kwenye tasnia ya muziki huo licha la muziki huo kushuka.

LEAVE A REPLY