Khadija Kopa afunguka wasanii wa Taarab kumuogopa

0
250

Mwanamuziki wa Taarab nchini, Khadija Kopa amedai kuwa wasanii wenzake wa muziki huo wanamuogopa baada ya kutojibu baadhi ya nyimbo zake.

Khadija Kopa amewachana wasanii wenzake wa taarabu na kudai kuwa wanamuogopa ndio maana hawawezi kutunga nyimbo zenye vijembe vinavyojibu nyimbo zake kama ilivyokuwa zamani.

Hivyo mwanamuziki huyo kawataka waache uoga wafanye wafanye ushindani ili taarabu iweze kufika mbali.

Khadija Kopa alifunguka hayo kwenye mahojiano aliyofanya na kituo cha televisheni cha East Africa ambapo alizidi kufunguka.

Kwasasa mziki wa Taarab umeonekana kupoteza ladha yake iliyokuwepo kama zamani na hata kupungua kwa mashabiki huku mashabiki wengi kudai taarab ilipoa baada ya Mzee Yusuph kustaafu.

LEAVE A REPLY