Kesi ya Wema yapigwa kalenda

0
143

Kesi ya mwanadada Wema Sepetu ya kurekosi na kujipiga picha akiwa faragha na mpenzi wake bado inaonekana kuwa nzito hasa baada ya kesi hiyo kushindwa kuendelea kusomwa mahakamani kwa madai kuwa uchunguzi wa kesi iyo bado haujakamilika.

Wema ambae anakabiliwa na kesi hiyo amekuwa akitakiwa kwenda katika mahakama ya Kisutu kila mara kesi yake inaposomwa.

Akiongea mbele ya mahakama, wakili wa kesi hiyo anasema kuwa kesi hiyo ilipangwa kusoma lakini haitawezekana kwa sababu upepelezi haujakamilika.

Wema amekuwa na mwaka mbya mwaka huu hasabaada ya kukumbwa na kesi moja baada ya nyingie, kama itakumbukuwa mwanadada huyo aliweza kusota na kesi ya madawa ya kulevya kwa mwaka mzima na hata baada ya hukumu kutoka alitakiwa kulipa faini ili asiweze kwenda jela.

Lakini hata baada ya kupambana na kesi ya madawa ya kulevya sasa limekuja lingine la kumfanya asote tena mahakamani ambalo ni kosa la kimtandao.

LEAVE A REPLY