Kesi ya Wema Sepetu yapigwa kalenda

0
114

Kesi ya kusambaza picha za ngono mtandaoni inayomkabili muigizaji wa Bongo Movie, Wema Sepetu imeahirishwa hadi Disemba 12 mwaka huu kutokana na upelelezi kutokamilika.

Wema amefika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kusikiliza kesi inayomkabili ambapo anashtakiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa tuhuma za kuchapisha na kusambaza video za maudhui ya ngono mitandaoni.

Novemba mosi mwaka huu Wema alipandishwa katika mahakama hiyo akikabiliwa na shtaka la kusambaza video  ya ngono kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram.

Wema Sepetu alisambaza mitandaoni video zake za faragha akiwa na mpenzi wake, anayejulikana kama PCK.

Kesi hiyo imeahirishwa leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam ambapo itasikilizwa tena Desemba 12 mwaka huu kutokana na upelelezi wa kesi hiyo kutokamilika.

LEAVE A REPLY