Kesi ya Wanafunzi wa chuo cha St. Joseph kusikilizwa Februari 15

2
193

Kesi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha St. Joseph waliorudishwa nyumbani kwa kukosa sifa kutokana na vigezo vya Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) kufanyika Februari 15 mwaka huu.

Mahakama Kuu inatarajia kufanya usuluhishi huo katika kesi ya madai ya Sh bilioni 6 iliyofunguliwa na wanafunzi 316 waliokuwa wakisoma chuo hicho.

Awali usuluhishi ulitakiwa kufanyika Januari 23 mwaka huu mbele ya Jaji Rose Temba, lakini ulipangiwa tarehe nyingine ambapo sasa utafanyika Februari 15 kwa sababu ya kusubiri mwongozo kutoka kwa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako.

Katika usuluhishi huo, wizara hiyo inawakilishwa na wakili Anna Kalomo  ambaye aliomba waziri huyo aipitie na atoe mwongozo wake ili maamuzi mazuri yaweze kufikiwa.

TCU inawakilishwa na Rose Rutha, St. Joseph  inawakilishwa na wakili Jerome Msemwa huku wanafunzi wakiwakilishwa na wakili, Emmanuel Muga.

Kwa utaratibu wa mahakama endapo usuluhishi huo utashindikana,  kesi ya msingi ambayo ipo mbele ya  Jaji Winfrida Koroso itaanza kusikilizwa.

Katika kesi hiyo, wanafunzi wanne Ramadhan Kipenya, Inocent Peter , Faith Kyando na Mohammed Mtunguja waliruhusiwa kuwawakilisha wenzao mahakamani hapo.

2 COMMENTS

    • @Kinembwe, Florian…ni kweli February 15 haijafika na ndio maana hiyo habari imeandikwa ‘itasikilizwa tarehe 15’ na haijaandikwa ‘imesikilizwa’ au ‘ilisikilizwa’. Ahsante kwa kutembelea @IshiKistaa.com na ahsante kwa maoni yako

LEAVE A REPLY