Kesi ya viongozi wa Chadema yaanza kusilizwa

0
177

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo imeanza kusikiliza kesi dhidi ya Mbowe na viongozi wenzake wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo ambapo wanakabiliwa na mashitaka ya kufanya mikusanyiko isiyo halali.

Viongozi wa chama hicho waliofika mahakamani hapo akiwemo Mbowe, ni Peter Msigwa, Salum Mwalimu, John Mnyika, Esther Matiko, Dk. Vicent Mashinji.

Wabunge Halima Mdee na Ester Bulaya hawakufika mahakamani hapo kutokana na kilichoelezwa na wakili wao, Peter Kibatala, kuwa ni matatizo ya usafiri.

Viongozi hao wa CHADEMA wanakabiliwa na mashtaka 12 katika hiyo ya  kufanya mkusanyiko na maandamano yasiyo halali  Februari 16, 2018 yaliyosababisha kifo cha aliyekuwa mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwiline.

LEAVE A REPLY