Kesi ya Scorpion hadi Januari 25 baada ya Daktari kushindwa kutokea mahakamani leo

0
396

Daktari aliyemtibu Said Mrisho aliyetobolewa macho na Scorpion ameshindwa kufika mahakamani kutoa ushahidi mpaka kupelekea kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha inayomkabili Salum Njwete ‘Scorpion’ kushindwa kuendelea leo.

Scorpion alifikishwa mahakamani hapo saa mbili na nusu akitokea Gereza la Ukonga na kuhifadhiwa kwa muda kwenye mahabusu ya mahakama hiyo.

Kesi hiyo ilianza kusikilizwa saa tatu ambapo Wakili wa Scorpion, Juma Nasoro, Wakili Mwandamizi wa Serikali, Nasoro Katuga, Hakimu anayeendesha kesi hiyo, Frola Haule na makarani wote walikuwa tayari kwenye chumba inapoendeshwa kesi hiyo wakimsubiri mtuhumiwa huyo apelekwe ili kesi iendelee.

Scorpion akiwa kizimbani, Wakili Katuga aliiambia mahakama hiyo kuwa kesi hiyo ilifika mahakamani hapo kwa ajili ya shahidi wa nne upande wa Jamhuri ambaye ni daktari aliyemtibu majeruhi kutoa ushahidi wake.

Wakili huyo amesema shahidi huyo alitoa udhuru mahakani hapo kuwa asingeweza kufika mahakamani hapo kwa kuwa yuko nje ya kituo cha kazi hivyo ameomba kesi hiyo iahirishwe na shahidi huyo apewe wiki mbili au tatu.

Baada ya ombi la wakili huyo, mahakama hiyo iliahirisha kesi hiyo mpaka Januari 25 mwaka huu ambapo Scorpion alirudishwa rumande.

Picha kwa hisani ya Global Publishers

LEAVE A REPLY