Kesi aliyofungua Mobeto dhidi ya Diamond kuanza kusikilizwa Oktoba 30

0
291

Mwanamitindo wa Bongo, Hamisa Mobeto amemfungulia kesi Diamond kwa madai ya kushindwa kumuomba radhi na kutotoa matunzo ya mtoto.

Wito huo wa Diamond umewasilishwa na mawakili wa Mobeto, Abdullah Zulu na Walter Godluck kutoka Kampuni ya Uwakili ya Century Attorneys.

Diamond Platnumz anadaiwa kumdhalilisha na kutompa matumizi ya mtoto kwa takribani miezi miwili.

Wakili Zulu amesema mteja wao Hamisa Mobeto alimtumia Diamond notisi ya kumuomba radhi na kumtaka apeleke matunzo ya mtoto ndani ya siku saba.

“Baada ya kuona kimya tulipeleka kesi katika Mahakama ya Kisutu upande wa watoto  (The Juvenile Court Of Dar es Salaam).

Kesi hiyo inatarajiwa kuanza kusikilizwa rasmi Oktoba 30, mwaka huu katika Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam.

 

LEAVE A REPLY