Kenya: Madaktari waanza mgomo wa nchi nzima

0
134

Madaktari nchini Kenya wameendela na mgomo wa nchi nzima wa kuishinikiza serikali kuwalipa stahiki zao licha ya polisi kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya madaktari waliokuwa kwenye vikundi.

Madaktari hao waliokuwa wakiandamana kwenye mji mkuu wa Nairobi huku wakiimba nyimbo za ukombozi pamoja na kubeba mabango yenye ujumbe mbalimbali wanataka serikali iwalipe stahiki ambazo tayari serikali ilikubali kuwalipa tangu mwaka 2013.

Madaktari hao wamekuwa wakitumia kalu mbiu zinazonasibishwa na kashfa za rushwa zilizoikumba serikali ya rais Uhuru Kenyatta katika siku za karibuni ili kuonyesha kuwa serikali ina uwezo wa kuwalipa stahiki hizo.

Wakati mgomo huo ukiendelea, wagonjwa wa akili kutoka hospitali ya Mathare nao wametumia mwanya wa kukosekana kwa waangalizi wao na kutoroka kwenye hospitali hiyo.

mgomo-wa-madaktari-kenya

madaktari-wagoma-kenya

LEAVE A REPLY