Kenya Airways yapata hasara kubwa

0
103

Shirika la ndege la Kenya, Kenya Airways limetangaza kupata hasara ya KSH 26bn sawa na TZS 573bn kwa mwaka wa fedha uliomalizika mwezi Machi mwaka huu.

Shirika hilo linalojinadi kwa kauli mbiu ya FAHARI YA AFRIKA limepata hasara hiyo huku mpinzani wake wa kibiashara, shirika la ndege la Ethiopia likitangaza kupata faida ya KSH 17bn sawa TZS 382bn na   katika kipindi hicho hicho kinachoishia mwezi Machi.

Mashirika ya ndege ya Kenya na jirani yake Tanzania yamekuwa kwenye msukosuko wa uchumi kwa muda mrefu huku shirika la ndege la Tanzania ‘Air Tanzania’ likishindwa kutoa huduma kwa muda mrefu sasa.

Mashirika hayo yamedaiwa kusumbuliwa na matatizo ya utawala na ushindani mkubwa katika soko.

Shirika la ndege la Kenya husafiri kwenye vituo 54 duniani ambapo kati ya hivyo vituo 44 ni vituo vya ndani ya Afrika.

Kwa upande wake, serikali mpya ya Tanzania imedhamiria kulifufua shirika lake la ndege na kuanza tena safari za anga na tayari imeshalipia 40% ya manunuzi ya ndege mpya mbili.

LEAVE A REPLY