Kendrick Lamar apata mtoto wa kike

0
299

Mwanamuziki wa hip hop kutoka nchini Marekani, Kendrick Lamar  amefanikiwa kupata mtoto wake wa kwanza mwezi huu baada ya kuficha siri katika kipindi chote cha ujauzito wa mchumba wake, Whitne Alford.

Msanii huyo alimkaribisha duniani mtoto huyo wa kike aliyempata na mchumba wake Whitney aliyekuwa nae kwenye uhusiano kwa miaka sasa.

Wawili hao  walikutana  miaka 10 iliyopita ambapo walificha mahusiano hayo  hadi walipoamua kuyaweka kuweka wazi  Aprili 2015.

Sikuweza hata kumwita ni mke wangu. Nilimuona kama rafiki mwema zaidi kwangu. Kifupim  ni mtu ambaye nina uwezo wa kumwelezea hofu zangu na akanielewa,” alisema Kendrick.

Miezi saba baadaye, mshindi huyo wa tuzo ya Grammy alithibitisha kuwa yeye na Whitney waliingia kwenye uchumba.

LEAVE A REPLY