Kayumba akataa kuzungumzia mtoto wake

0
142

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Kanyumba ambaye alikuwa ni mshindi wa BSS mwaka 2015 amekanusha kutelekeza mtoto kama taariza zilivyosambaa katika mitandao ya kijamii.

Siyo hali ya kawaida kwa mzazi kuacha kumuongelea mtoto wake kama hakuna tatizo, na habari ilizonazo eNewz ni kwamba msanii huyo amemkimbia mtoto na kususa malezi kwa kile alichodai kwamba muziki bado haumlipi, hata hivyo Kayumba aligoma kabisa kuongelea tuhuma hizo na kusema hawezi jibu kitu chochote kwa wakati huu.

 

“Sidhani kama kuna umuhimu wowote wa mashabiki kujua maisha yangu, binafsi ninachofahamu ni kwamba mashabiki zangu wanapaswa kupata muziki mzuri kutoka kwangu ila mambo ya familia sio vyema wao kuyafahamu kwanza yanaweza yakawafanya wakaacha kufuatilia muziki wangu kwa kuwa hawajawahi kusikia nikizungumzia maisha yangu binafsi tangu wamenifahamu.

 

Hata hivyo Kayumba alisema kwa sasa anahitaji sapoti ya mashabiki zake katika muziki wake kwa kuwa bila wao yeye hawezi kufanya chochote na amewaambia wategemee mambo mazuri kutoka kwake kwa upande wa muziki ila kwa sasa kuna video yake mpya ambao amefanya na Director Snaipa.

LEAVE A REPLY