Kauli ya Irene Uwoya kuhusu Msami

0
198

Muzigizaji wa Bongo Movie, Irene Uwoya amekanusha kuendelea kuwa kwenye mapenzi na mwanamuziki wa Bongo Fleva, Msami kama watu wanavyodhani.

Kauli hiyo ya Uwoya imekuja kufuatia Msami kueleza kuwa hawajawahi kuachana kimapenzi, msanii wa Bongo Muvi, Irene Uwoya ameibuka na kupinga vikali kauli hiyo.

Uwoya amesema hadhani kama mwanamuziki huyo alimaanisha hawajaachana kimapenzi, bali ni kwenye kuzoeana au kukutana na kupiga naye stori lakini siyo kuhusiana na mapenzi kama wengi walivyodhani.

“Nafikiri Msami alizungumzia kuhusu ukaribu wetu wa siku zote, lakini sidhani kama ni ishu ya mapenzi na kama ni ukweli wala asingezungumzia hivyo hadharani. Kikubwa ni kwamba Msami anapenda tu kampani yangu,” alisema Uwoya.

Msami wa Irene Uwoya walikuwa kwenye mahusiano siku za nyuma kabla ya wawili hao kuachana na kila mmoja kuanzisha mahusiano mengine katika maisha yao.

LEAVE A REPLY