Kauli ya Ibraah baada ya Killy na Cheed kujiunga Konde Gang

0
34

Mwanamuziki wa Bongo fleva, Ibraah kutoka Konde Gang amesema hajaumia wasanii wengine ambao ni Cheed na Killy kuongezeka kwenye lebo yao kama ambavyo watu wanasema mitandaoni.

Ibraah amesema ujio wa Cheed na Killy utampa changamoto mpya na nguvu ya kupambana zaidi hasa ukizingatia wao ni wasanii wazuri wenye vipaji vya kuimba na kuandika mashairi kwahiyo kwake anawachukulia kama Neema.

“Naona mitandaoni watu wanasema sijui nimeumia Cheed na Killy kusainiwa Konde Gang, hata wakati nasainiwa mimi nilijua ipo siku wataongezeka wasanii wengine kwa sababu Harmonize amekusudia kusaidia vijana wenzake wenye vipaji, na bado wataendelea kuongezeka.

“Nawaomba mashabiki wangu wawasapoti Cheed na Killy kama wanavyonisapoti mimi, mwisho wa siku tunakuza muziki wa Tanzania” amesema Ibraah

Siku mbili zilizopita kupitia ukurasa wake wa Instagram, Harmonize na menejiment yake waliwatangaza rasmi Cheed na Killy kuwa ni wasanii wapya katika lebo yao.

Kabla ya kutambulishwa katika Lebo ya Konde Gang, Cheed na Killy, walikuwa ni wasanii wa mwanamuziki Alikiba kwenye lebo yake ya Kings Music.

LEAVE A REPLY