Kauli ya Dully Sykes kuhusu kuoa

0
126

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Dully Sykes amefunguka mambo mawili ambayo ni mipango yake ya kufunga ndoa na kuhama kwa wasanii ambao aliwahi kuwasaidia katika muziki.

Dully Sykes amesema atasubiri  mke bora kutoka kwa Mungu, kama alivyofanya ndugu yake Q Chief ambaye ameoa siku kadhaa zilizopita.

“Inshaalah nitafunga ndoa na mke bora analetwa na Mungu kwa sababu ndoa huipangi wewe inapangwa na Mungu, ukitaka kujipangia mwenyewe utaoa leo kesho utaacha, kwahiyo mimi nitakuwa kama ndugu yangu Q Chief nasubiri Mungu aniletee jiko nitaoa”amesema Dully Sykes.

Akizungumzia kuhusu kuwasaidia wasanii ambao wamewahi kupita katika mikono yake na kuondoka amesema, “Wasanii ambao wamepita kwangu na kuondoka nilikuwa sijaandikishana nao mikataba na sikuwaambia wakae kwangu milele, wakitoka huwa naona ni kitu cha kawaida tu”.

LEAVE A REPLY