Kitabu cha Harry Potter kuuzwa kwa 1.3bn

0
178

Toleo maalum la kitabu cha Harry Potter kilichoandikwa kwa mkono na mwandishi JK Rowling ambacho hakijawahi kuchapishwa kinatarajia kuuzwa kwa £500,000 (TZS 1.3bn) na mmiliki wake wa sasa, Barry Cunningham.

Kitabu hicho chenye kava iliyonakshiwa na madini kiitwacho The Tales of Beedle the Bard kinatarajiwa kuingizwa mnadani jijini London mwezi ujao.

JK Rowling anadaiwa kumpatia kitabu hicho Cunningham, baada ya kukubali kumchapishia kitabu chake cha kwanza cha Harry Potter.

Nakala ya kitabu hicho inajumuisha maandishi ya mkono ya Rowling pamoja na michoro aliyoichora kwa mkono pia.

Mwandishi huyo ameandika kwenye kitabu hicho maneno:

‘To Barry, the man who thought an overlong novel about a boy wizard in glasses might just sell… THANK YOU’.

Nakala ya kitabu hicho ni moja ya nakala saba za kipekee zilizopo huku nakala sita zikiwa zimegawiwa kwa marafiki huku nakala ya saba ikiuzwa kwenye mnada kwa £1.95m (TZS 5.3bn) mwaka 2007.

rowlinginscriptionsothebys

potterjewel

LEAVE A REPLY