Katibu mkuu wa Basata awataka mashabiki kumtia moyo Nandy

0
255

Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), Godfrey Mngereza amesema mwanamuziki Nandy ambaye picha zake za utupu zilivuja anahitaji kupewa moyo kwa kuwa tukio hilo limemuumiza.

Mngereza amesema jamii iache kumlaumu mwanamuziki huyo, kwani kilichompata kinaweza kumtokea yeyote hasa katika ulimwengu huu wa sayansi na teknolojia.

Pia amesema kama Baraza wamemuita na kuongea naye kwa ajili ya kumpa moyo na kueleza hayupo katika hali nzuri kwa sasa na anahitaji kupatiwa ushauri wa kisaikolojia.

Siku mbili zilizopita video ya utupu ya mwanamuziki, Nandy ilisambaa katika mitandao ya kijamii akiwa na mwanamuziki mwenzake, Bilnass.

LEAVE A REPLY