Kapombe yupo fiti kuikabili Yanga

0
196

Beki wa kulia wa Azam FC, Shomari Kapombe amesema kwamba afya yake inaendelea vizuri baada ya kufanikiwa kurejea uwanja na kuanza mazoezi mepesi huku akiisubili mechi dhidi ya Yanga SC.

Beki huyo amerudi uwanjani baada ya kukaa nje kwa siku 122 kutokana na kusumbuliwa na mishipa ya damu kwenye mapafu lakini sasa amepona na kurejea kwa kaunza kufanya mazoezi mepesi.

Mchezaji huyo mpaka sasa amecheza mechi mbili za kirafiki na timu yake hiyo ikiwa dhidi ya JKT Ruvu na pamoja na Ruvu Shooting ambapo mchezo huo ulichezwa siku ya jumamosi.

Beki huyo amesema kwamba kwasasa anajiweka fiti kwa ajili ya mchezo wa ngao ya jamii dhidi ya Yanga SC utakaochezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Agosti 17 mwaka huu.

Azam FC inatarajia kucheza mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga SC ikiwa ni ufunguzi wa ligi kuu Tanzania Bara Agosti 17 mwaka huu katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

LEAVE A REPLY