Kanye West na Kim Kardashian watarajia mtoto mwingine

0
88

Wanandoa Kim Kardashian  na Kanye West wamethibitisha kwamba mtoto wao ajaye ni mwanamme.

Wawili hao ambao wana watoto watatu —  North mwenye umri wa miaka mitano, Saint (3) na Chicago (miezi 11)  — wamemtumia mwanamke mwingine kubeba mimba hiyo ili kupata mtoto mwingine.

Akizungumza katika kipindi cha televisheni cha ‘Watch What Happens Live’ Jumatatu, Kim alithibitisha kwamba watapata mtoto wa kiume “hivi karibuni”.

Alipoulizwa na mtangazaji Cohen iwapo alikuwa anategemea mtoto mwingine, Kim alikubali japokuwa alikiri aliwahi kufichua jambo hilo kwa bahati mbaya wakati wa Krismasi mwaka jana kwani alikuwa amelewa kinywaji.

Wakati akiwa na ujauzito wa North na Saint, Kim alipata matatizo ya uzazi hivyo yeye na Kanye waliamua kumtumia mwanamke mwingine kubeba mimba ya mtoto wao wa tatu ambayo ilimzaa binti yao, Chicago.

LEAVE A REPLY