Kanye West kuja na bidhaa ya viatu vya yeboyebo

0
109

Mwanamuziki nyota wa Marekani, Kanye West anatarajia kuja na bidhaa zake mpya za viatu aina ya Yeboyebo.

Katika ukurasa wake wa Instagram, Kanye alianika aina hiyo ya viatu vya yeboyebo kuwa ni Yeezy Slides ambayo imetengenezwa kwa ‘material’ ya plastiki.

Hata hivyo, rapa huyo alipata makavu ya kutosha mara baada ya kuweka yeboyebo hizo mtandaoni huku wengine wakimwambia hayupo siriazi na wengine wakisema viatu hivyo labda akawauzie wafungwa.

Kanye kwa kushirikiana na mkewe, Kim Kardashian, mwaka jana kwao ulikuwa wa mafanikio baada ya kutoka na viatu vya Yeezy pamoja na makoti ya Faux ya watoto.

LEAVE A REPLY