Kanye West awaomba radhi Beck na Bruno Mars

0
362

Staa wa muziki kutoka Marekani, Kanye West ameonyesha ustaarabu unaopaswa kuigwa na mastaa wenzake kwa kukubali kuwaomba radhi wanamuziki wenzake mastaa Beck na Bruno Mars.

Kupitia mtandao wa Twitter, West aliandika ‘I would like to publicly apologize to Beck. I’m sorry Beck’, ‘Napenda kuomba radhi kwa Beck mbele ya kadamnasi . Samahani Beck’.

West aliwa-diss mastaa hao kwenye mfululizo wa tweets ambazo alizituma kwa wasanii mbalimbali.

West alipanda jukwaani wakati wa utoaji wa tuzo za Grammy na kuidhihaki tuzo aliyoshinda Beck ya Albam bora ya mwaka.

Kwenye mahojiano aliyofanyiwa siku za karibuni, West alimtaka Beck ‘aheshimu usanii’ na ampe tuzo ya albamu bora ya mwaka msanii Beyonce.

KANYE WEST Becky

KANYE WEST - Beyonce

Kanye west - Bruno Mars

Tabia hiyo ya West inaonekana kujirudia ambapo mwaka 2009 alipanda jukwaani na kumpokonya Beck kipaza sauti na kudai tuzo aliyoshinda msanii Taylor Swift ilipaswa kuchukuliwa na Beyonce.

Hata hivyo mastaa aliowaomba msamaha, Beck na Bruno Mars bado hawajamjibu.

LEAVE A REPLY