Kanye West amlipa Kim Kardashian bilioni 2 asifanye tangazo

0
77

Mwanamuziki nyota wa Marekani, Kanye West amemlipa mke wake Kim Kardashian kiasi cha dola milioni $1 ambayo ni sawa na bilioni 2 za Tanzania baada ya kumzuia kuposti tangazo kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Kim amesema kuwa wiki moja kabla ya siku ya Mama duniani alitafutwa na kampuni kubwa ya mavazi nchini Marekani ikimtaka aposti picha moja ya tangazo kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii na itamlipa dola laki 9.

Kim amesema yeye aliona ni fedha nyingi lakini ilimpasa aombe ushauri kwa mumewe, lakini Kanye West akamkatalia kufanya hivyo.

Hata hivyo, wiki mbele baadae May 12 mwaka huu siku ya Mama Duniani, Kanye alimtumia Kim maua na bahasha iliyokuwa na hundi (cheque) ya dola milioni 1.

Lakini Kim hajaelezea sababu ya kukatazwa kuposti tangazo hilo na mume wake huyo kwenye ukurasa wake wa Instagram.

LEAVE A REPLY