Kampuni ya simu ya TTCL yafutwa na sasa kujulikana kama Shirika la TTCL

0
121

Kampuni ya Mawasiliano Tanzania ya (TTCL) imebadilishwa na kuwa Shirika badala ya kampuni.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Makame Mbarawa, amesema kuwa anamshukuru sana Rais Magufuli kwa kuona umuhimu wa kuona wa kuwa na shirika la mawasiliano madhubuti kwa ajili ya kuleta maslahi mapana ya nchi, huku akitoa shukrani pia kwa Wabunge wote kwa kukubali kupitisha muswada huo.

Prof Mbarawa, amesema uwepo wa sheria ya shirika la mawasiliano unatoa fursa ya kuboresha sekta kwa kuweka mazingira mazuri ya usimamizi wa miundombinu ya mikakati chini ya shirika hilo.

Profesa Mbarawa pia amewajulisha watanzania wote kuwa mabadiliko ya kuhama kutoka kampuni kuwa shirika la mawasiliano hayatawaathiri kwa namna ya utoaji wa huduma mbalimbali ambazo zilikuwa zinatolewa na TTCL.

LEAVE A REPLY