Kamishna wa Idara ya uhamiaji awataka wananchi kushirikiana na idara hiyo

0
163

Kamishina Jenerali wa Idara ya Uhamiaji, Dkt. Anna Makakala amewataka wananchi wa Wilaya ya Karagwe kushirikiana na idara ya uhamiaji ili kuwabaini na kudhibiti wahamiaji haramu wanaoingia nchini kupitia vijiji vya Wilaya hiyo.

Jenerali Anna ameyasema hayo jana alipokuwa akihotubia wananchi wa kijiji cha Mugulika Kata ya Bwerenyange wilaya ya Karagwe Mkoani Kagera, ambako alitembelea kwaajili ya kujionea shughuli zinazotekelezwa na Idara yake.

Katika mkutano huo wa hadhara Jenerali Anna amesema wanaanchi lazima watoe ushirikiano kwa idara ya uhamiaji ili kwa pamoja waweze kudhibiti tatizo la wahamiaji haramu ambao baadhi yao huwa ni waharifu na husababisha madhara kwa wenyeji.

Aidha katika ziara hiyo Kamishina Jenerali Anna ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Karagwe Godfrey Mhaluka ambapo kwa pamoja wametembelea vichochoro na vipenyo ambavyo vinaelezwa kutumiwa sana na wahamiaji haramu kuingia nchini.

LEAVE A REPLY