Kala Jeremiah autaka urais

0
37

Mwanamuziki wa Hip Hop, Kala Jeremiah amesema akiingia kwenye siasa hatamani kuwa Mbunge bali anataka kuwa Rais wa Taifa hili kwa sababu anaijua nchi nje ndani.

Kala Jeremiah amesema akiwa Rais ataleta mabadiliko ambayo anaona yatafaa pia tayari ana wimbo unaoitwa ningekuwa Rais aliozungumzia masuala mengi juu ya uongozi.

Kala amesema kuwa Mwaka 2010, 2015 na 2020 nimeombwa sana kugombea Ubunge mpaka vijana wananifuata nyumbani kutaka kunichukulia fomu lakini utayari ninanukuwa sina.

Pia amesema kuwa nitakapokuwa ninaingia kwenye siasa sitamani kuwa Mbunge nitaingia kwa sababu nataka kuwa Rais wa Nchi, nitaleta mabadiliko ninayoyaona mimi na naijua nchi nje ndani”.

Mwanamuziki huyo amekuwa na ndoto ya kuwa rais wa Tanzania kwa kuwa anajua changamoto za maisha ya watanzania kwa ujumla.

LEAVE A REPLY