Kala Jeremiah atembelea alipouza mitumba

0
81

Mwanamuziki wa Hip Hop nchini, Kala Jeremiah ametembelea mahali ambako alikuwa akifanya kazi ya kuuza nguo za mitumba, kazi ambayo alikuwa akiifanya kabla ya kutoka kimuziki.

Kala Jeremiah ameitaja sehemu hiyo maarufu kama “Mlango mmoja” iliyopo jijini Mwanza kuwa ndipo mahali ambako alifanya kazi hiyo kwa muda wa miaka mitatu.

 “Jana nilifanikiwa kuingia mlango mmoja au langolango sehemu niliyokuwa nikiuza mitumba jijini Mwanza, nimefurahi kuwaona rafiki zangu ambao nilifanya nao biashara kwa miaka 3 japo kuna wengi sikuwakuta kutokana na kuwa jana ililiwa jumapili. Nimesikitika sana kuona nusu ya soko limeungua na kusababisha hasara kubwa sana,.

“Nawaombea kwa mungu ndugu zangu awape wepesi katika kipindi hiki kigumu. Pia naziomba mamlaka zinazohusika ziharakishe namna ya urudishiaji wa soko hili muhimu sana na lililoajiri vijana wengi sana na linategemewa sio Mwanza tu bali Kanda yote ya Ziwa,”.

Pia Kala Jeremiah ametumia nafasi ya kutembelea sehemu hiyo kwa kutoa historia fupi ya maisha yake wakati anauza mitumba eneo hilo.

LEAVE A REPLY