Kala Jeremiah anasurika kupata ajali

0
21

Mwanamuziki wa Hip Hop Bongo, Kala Jeremih amefunguka kusema wamenusurika kupata ajali na Sholo Mwamba wakiwa safarini kurejea Dar Es Salaam wakitokea Jijini Dodoma.

Tumenusurika ajali tulikuwa kwenye speed tukasikia kishindo nikajua tairi limebast kumbe ni diff imekula bearing ambayo ikakata mawasiliano ya tairi, tunashukuru Mungu dereva akai-control gari vizuri tukajikuta tunaning’inia kwenye ukingo wa barabaraamesema Kala Jeremiah 

 Aidha ameongeza kusema “Nilikuwa mimi Sholo Mwamba, meneja wake, Dj Tittoh na dereva wetu ambaye tunajiuliza tumpe zawadi gani kama kamati, kwa jinsi watu waliyoona walisema sio dereva wa nchi hii, kilichotokea pale kuokoka ilikuwa kama ni mkono wa Mungu tu”.

Mwezi Septemba mwaka huu wasanii wengine ambao ni Belle 9, Lulu Diva na Bonge la Nyau walipata ajali ya gari maeneo ya Chalinze wakati wanarejea Dar Es Salaam wakitokea Iringa kwenye kampeni za Chama Cha Mapinduzi.

LEAVE A REPLY