Kala Jeremiah akanusha kuwa na bifu na Roma

0
271

Mwanamuziki wa hip hop Bongo, Kala Jeremiah amekanusha tetezi zilizosambaa katika mitandao ya kijamii kuwa ana bifu na mwanamuziki mwenzake wa Bongo Ibrahum Mussa maarufu kama Roma Mkatoliki.

Kala amesema kuwa hana tofauti na Roma ni habari zinazosambazwa katika mitandao ya kijamii kwa ajili ya kuwagombanisha lakini hawana tofauti kabisa.

Kala amesema kuwa hawezi kugombana na Roma kwakuwa anamchukulia kama ndugu yake kutokana na kufanya kazi pamoja hivyo hawana tofauti hata kidogo.

Pia Kala amesema kuwa kwasasa haonekani na Roma wakiwa pamoja kwakuwa kila mmoja yupo bize na kazi zake isitoshe Roma kwa kwasasa yupo na kundi Rostam akiwa na Stamina.

Kala na Roma walifanya kazi za pamoja ikiwemo ‘Nchi ya Ahadi’ ambayo ilifanya vizuri sana miaka ya nyuma.

LEAVE A REPLY