Kaka wa kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Nam ameuawa nchini Malysia

0
196

Ndugu wa kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un, anayeitwa Kim Jong Han amefariki dunia akiwa nchini Malysia baada ya kuvamiwa na watu wasiojulikana.

Taarifa zilizosambaa sehemu mbali mbali zinasema kuwa chanzo cha kifo chake ni mauaji dhahiri yaliyotokea katika uwanja wa ndege wa Kuala Lumpur nchini Malaysia.

Polisi nchini Malysia wamesema kwamba Kim Jong Nam alishambuliwa siku ya Jumatatu wakati anasafiri kuelekea Macao nchini China.

Kabla hajafariki dunia wakati akipelekwa hospitalini, alitoa maelezo kuwa alivutwa kutoka kwa nyuma na kumwagiwa kimiminika usoni mwake.

Uchunguzi wa kitabibu utafanywa ili kuweza kubaini chanzo cha kifo huku kukiwa na tetesi kuwa huenda kimiminika alichomwagiwa usoni huenda ikawa ni simu.

Chanzo kutoka katika serikali ya Marekani kinasema kwamba wanaamini kwa dhati kuwa bwana Kim, aliyekuwa anaishi uhamishoni ameuawa na mawakala kutoka Korea Kaskazini.

LEAVE A REPLY