Kajala amwagia sifa Harmonize

0
195

Muigizaji wa Bongo Movie, Kajala Masanja amemmwagia sifa mpenzi wake mwanamuziki wa Bongo Fleva, Harmonize.

Harmonize aliweka wazi mahusiano yake na Kajala Februari 14 ,2021 na tangu kutokea kwa sakata hilo amekuwa naye bega kwa bega ikiwemo kwenda polisi kufikisha malalamiko kuhusu waliohusika na jambo hilo.

Harmonize aliandika waraka mrefu wa kumtuhumu Rayvanny kwa kitendo alichofanya kwa binti huyo wa miaka 19 na kutaka hatua zaidi za kisheria zichukuliwe dhidi yake.

Kajala kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa Instagram ameandika: “Wewe ni kitu kizuri ambacho sijawahi kuwa nacho”.

Kajala ameandika hayo huku akiwa ameweka picha inayowaonyesha wakivinjari visiwa vya Zanzibar ilhali wakiwa  wameshikana mikono na Harmonize, na pembeni wakiwa wanalindwa na walinzi wa msanii huyo.

LEAVE A REPLY