Kajala akanusha kuvunja ndoa ya P-funk Majani

0
406

Muigizaji wa Bongo Movie, Kajala Masanja amekanusha madai ya kuvunja ndoa ya Producer wa Bongo Records P-Funk Majani ambaye ni mzazi mwenzake.

Kajala amekanusha kuvunja ndoa ya P Funk na mkewe Samira huku akidai kuwa hayo ni mambo ya mitandaoni tu wala hayana ukweli wowote.

“Mimi sijavunja ndoa ya P Funk, yule ni mzazi mwenzangu, nimeishi naye miaka tisa, nimezaa naye mtoto (Paula) ambaye sasa hivi yupo kidato cha nne na ana miaka 16.

Taarifa za Kajala kuvunja ndoa ya P Funk na Samira iliibuka baada ya ukaribu wa wawili hao wa hivi karibuni.

LEAVE A REPLY