Kajala akanusha kushika ujauzito wa P-Funk Majani

0
237

Muigizaji wa Bongo Movie,  Kajala Masaja ‘Kay’ amekanusha kushika ujauzito wa aliyekuwa mpenzi wake prodyuza P Funk Majani.

Kajala ameema kuwa amekuwa akiona maneno mengi kwenye mitandao ya kijamii kuhusu ishu hiyo, jambo ambalo anashindwa kuelewa limetokea wapi.

“Jamani kwa nini watu wakimuona mtu amenawiri kidogo wanasema kuhusu mambo ya ujauzito? Mimi na P (Funk) mbona wanatung’an’ganiza sana? Wanashindwa kuelewa kabisa yule ni mzazi mwenzangu?” Alihoji Kajala akisisitiza kuwa hana kibendi.

Minon’gono ya Kajala kunasa ujauzito wa P Funk iliibuka baada ya ukaribu wa wawili hao wa hivi karibuni. Kajala na P Funk wana mtoto mkubwa aitwaye Paula.

LEAVE A REPLY