Kajala afungukia video ikimuonesha akicheza na Paula

0
142

Muigizaji wa Bongo movie Kajala Masanja ameibuka na kujitetea Baada ya video iliyomuonyesha akikata mauno na binti yake Paula kusambaa kwenye Mitandao ya kijamii.

Kajala alisema kuwa video hiyo haikuwa na lengo baya kama watu wanavyomshambulia mitandaoni bali ilipigwa alipokuwa akicheza na mwanaye huyo kama kujifurahisha tu.

Watu wanatakiwa kujua video hiyo haina ubaya na wala haijavujishwa na mimi wala Paula, siku hiyo nilikuwa nyumbani nimelala kwani nilikuwa naumwa kwa muda mrefu.

Akaja Paula na rafiki yake msichana aliyekuwa akisoma naye akaniomba niamke ili nichangamke kidogo kwani alinionea huruma kwa kukaa kwangu ‘siriasi’.

Basi tukaweka muziki tukawa tunacheza kama mama na watoto wake. Baada ya hapo yule rafiki wa Paula alirekodi video na kuitupia kwenye group la wanafunzi wa shuleni kwao na kuiwekea maneno kuwa anatamani kuwa na mama kama mimi.

Hapo ndipo watu wakaanza kurushiana na mwisho ndiyo ikafika kwenye mitandao ambako imezua mjadala mbaya”.

Kajala amesisitiza  kuwa video hiyo haikuwa na nia mbaya au hakutaka kumkuza mwanaye mdogo kama wengi ambavyo wamekuwa wanadai bali ilikuwa ni katika kujifurahisha.

LEAVE A REPLY