Kajala achukizwa na kunenepa kwake

0
88

Muigizaji wa Bongo Movie, Kajala Masanja amefunguka na kuweka wazi kuwa anachukizwa sana na mwili wake ulivyokuwa kwa sasa baada ya kunenepa sana.

Kajala ameweka wazi kuwa kati ya vitu ambavyo anavichukia kwa sasa ni pamoja na mwili wake kuwa mnene kupitiliza.

Kajala amesema kuwa ubonge wake kwa sasa umefikia kiasi cha kumnyima raha kwani hata nguo zake nyingi ameshindwa kuzivaa kwa sababu hazimpiti mwilini.

Muigizaji huyo amesema kuwa kutokana na mwili wake kuwa mkubwa mpaka anahofia anaweza kupata presha au gonjwa lolote linalotokana na kunenepa.

Kajala ametangaza kuongezeka mwili kutokana na maisha ya stare he anayoishi kwa Hivi sasa hasa kutokana na mkataba Wake na Biko ambao unamuingizia mkwanja mrefu.

LEAVE A REPLY