Kagera Sugar yaitandika Simba 2-1 bila huruma leo

0
226

Kagera Sugar imefanikiwa kushinda 2-1 dhidi ya Simba kwenye mechi ya ligi kuu Tanzania Bara iliyofanyika katika uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera.

Simba ilionekana kutawala mchezo huo lakini wameshindwa kupata ushindi kwenye mechi hiyo kutokana na kutokuwa makini.

Goli la kwanza la Kagera Sugar limefungwa na Mbaraka yusuf katika dakika 28 ya mchezo huo baada ya kupiga shuti kali na kumshinda kipa wa Simba, Daniel Agyei na kutinga nyavuni.

Mshambuliaji Christopher Edward ndiye aliyeshinda goli la pili baada ya kuunganisha krosi iliyopigwa na beki wa pembeni wa Kagera Sugar.

Goli la kufutia machozi la Simba limefungwa na Mzamiru Yassin katika ya 60 ya mchezo huo baada ya piga nikpige kwenye lango la Kagera Sugar.

Kwa matokeo hayo Simba anabakiwa na pointi zake 55 akishika nafasi ya pili nyuma ya Yanga mwenye pointi 56 baada ya kushinda mechi ya jana dhidi ya Azam FC.

LEAVE A REPLY