Kada wa Chadema, Yeriko Nyerere akamatwa akiwa nyumbani kwake Kigamboni

0
337

Mwanachama wa Chadema, Yeriko Nyerere amekamatwa na watu wanaodhaniwa kuwa ni polisi au usalama wa taifa usiku wa kuamkia leo akiwa nyumbani kwake katika kijiji cha Mbutu kilichopo Kigamboni.

Taarifa iliyotolewa na Meya wa Ubungo, Boniface Jacob imesema kuwa Nyerere alikamatwa na watu hao ambao waliambatana na Mwenyekiti wa Kijiji cha Mbutu.

Amesema kuwa “Nimepata taarifa kutoka kwa ndugu wa Yeriko ambao wamenipigia simu alfajiri leo. Wamesema amekamatwa saa tisa usiku na watu hao ambao walivalia kiraia”.

Pia amesema kuwa Viongozi wa Chadema wanaelekea polisi kufuatilia kwa kina chanzo cha Yeriko kukamatwa,”.

Mwanachama huyo wa CHADEMA amekuwa maarufu katika mitandao ya kijamii kupitia post zake mbalimbali za kuikosoa serikali.

Source: Mwananchi

LEAVE A REPLY