Jux na Vanessa waipeleka Inlove & Money nchini Burundi

0
130

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Juma Jux amesema kuwa anatarajia kufanya ziara ya muziki ya Inlove & Money nchini Burundi akiwa na mpenzi wake Vanessa Mdee.

Wasanii hao ambao walipumzika kidogo baada ya kufanya ziara hiyo  ya kuwafikia mashabiki wao kwa mikoa kadhaa nchini wamemau akunza tena ziara hiyo huku wakisema kuwa kwa sasa itakuwa ni zaidi ya awali.

Pamoja na kwamba wawili hao wamkeuwa wapenzi lakini hii haiwazuii kufanya kazi pamona na kuchanganyana na wasanii wengine katika kufanya kazi.

Akiwakaribisha na kuwataarifu kwa kishindo kabisa , mashabiki zake wa burundi, mwanadada Vee amesema kuwa tamasha hilo linatarajiwa kufanyika March 3 mwaka huu.

Tamasha hilo lilifanikiwa sana nchini Tanzania mwaka jana ambapo walifanikiwa kuzunguka baadhi ya mikoa ya Tanzania na kupokelewa vizuri na mashabiki wao.

LEAVE A REPLY