Jux aweka wazi ulipaji wake wa kodi

0
60
Jux

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Juma Jux amesema kuwa yeye ni miongoni mwa wasanii wa Tanzania anayelipa kodi kubwa Serikalini kupitia biashara yake ya nguo.

 

Jux alikuwa anazungumzia mafanikio ya bidhaa zake za nguo za African Boy ambapo amesema kuwa amepata mafanikio makubwa kupitia mavazi yake hayo.

Jux ameendelea kusema kuwa “Mimi ni mmoja kati ya wafanyabishara na wasanii ambao wanalipa kodi kubwa, mimi kontena yangu moja nalipa tsh milioni 26 mpaka 27 na kwa mwaka naingiza kontena mbili mpaka tatu,”

Jux amesema kwa sasa ana duka la jumla Kariakoo Tanzania pamoja na Uganda huku akiwa na malengo ya kutanua biashara yake Afrika na duniani.

Muimbaji huyo amesema kwa sasa biashara hiyo anaimilili kwa asilimia mia moja huku akisema biashara ikitanuka na kuanza kuzaa matunda zaidi ataanza kuuza hisa.

 

LEAVE A REPLY