Jux aweka wazi mahusiano yake na Huddah

0
133
Jux

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Juma Jux amesema huwa ni ngumu sana wa kuchagua mwanamke wa kuwa naye kwenye mahusiano na mara nyingi huwa anakuwa na vigezo vingi sana.

Jux ameweka wazi kuwa yupo karibu na Huddah kwasababu wameshafanya kazi na wanawasiliana lakini kikazi zaidi.

”Huddah ana mahusiano yake japo mimi kwasasa sipo kwenye mahusiano lakini namheshimu Huddah na hatuna ukaribu huo ila huwa ananipa mawazo ya kazi” – Jux

Kuhusu kusumbuliwa na wasichana kwenye mitandao ya jamii, Jux amesema inatokea ila sio sana.

Kwa upande mwingine amesema mpenzi wake wa zamani Jackie Cliff, hajawasiliana naye muda mrefu ila anaweza kuwa anakaribia kutoka na kama atatoka wanaweza kuwa kwenye mahusiano ila itategemea.

LEAVE A REPLY